Hospitali ya Misheni ya Mbozi 

Hospitali ya Misheni ya Mbozi inamilikiwa na kanisa la Moravian nchini Tanzania – Jimbo la Kusini - Magharibi. Awali ilijulikana kama Hospitali ya Kanisa la Moravian, ilianzishwa mwaka 1961, kihistoria uilianzishwa na wamisionari wa kijerumani miaka ya 1940. Mmisionari mwanzilishi alikuwa Sr. Elizabeth Senft, aliyeanzisha kituo cha watoto yatima na kliniki ya wajawazito mwaka 1948, kufuatia wazo la Usharika wa Mbozi wa Kanisa la Moravian, ambaye alijenga kliniki ndogo iliyoezekwa kwa nyasi. Usharika wa Mbozi ulimpokea mchungaji mpya, Mch. Hartmunt Beck, ambaye baadaye mwaka 1960 alisimamia ujenzi wa majengo ya hospitali, huku akisaidiwa na mkandarasi Karl Madsen. Ujenzi ulikamilika mwaka 1961 na hospitali ilifunguliwa rasmi mwaka huo huo. Wamisionari waliendesha hospitali, huku wakiungwa mkono na wenyeji. Baadaye, mwaka 1974 serikali iliomba kuitumia hospitali hiyo kama hospitali teule ya wilaya, ilikubaliwa hadi mwaka 2001. Kisha hospitali ilirudishwa chini ya kanisa na kuanza kutambuliwa kama hospitali ya kujitolea.

Hospitali ya Misheni ya Mbozi ni miongoni mwa hospitali tano katika Mkoa wa Songwe yenye vitanda 150 na inahudumia wanajamii si chini ya watu 179,208. Hospitali nyingine ni pamoja na Hospitali ya Isoko katika Ileje, Hospitali ya Vwawa katika Mbozi, Hospitali ya Itumba katika Ileje na Hospitali ya Mwambani wilayani Songwe. Kutokana na huduma zake za kiwango cha juu na wafanyakazi waliobobea, hospitali hupokea wagonjwa kutoka sehemu zote za mkoa pamoja na mikoa mingine ya karibu.

Hospitali ya Misheni ya Mbozi ina matawi matatu ya huduma vijijini: zahanati ya Kapele, zahanati ya Iyendwe na kituo cha afya cha Nkanga. Magonjwa yanayoathiri watoto chini ya umri wa miaka mitano ni malaria, kichomi, maambukizi ya kwenye mapafu (Acute Respiratory Infection), na kuhara. Magonjwa yaliyokithiri miongoni mwa watu wazima ni malaria, meno, kutokwa na uchafu / usaa sehemu za siri (GDS) na kifafa.

Hospitali ya Misheni ya Mbozi pia, inasimamia kituo kidogo cha watoto yatima, karibu na hospitali. Kwa habari zaidi, tembelea linki ya chini.Miundombinu

Hospitali ina miundombinu mbalimbali kuanzia majengo hadi miundombinu ya kimawasiliano. Majengo ya hospitali ni pamoja na wodi, jengo la upasuaji, jengo la wagonjwa wa nje (OPD), maabara, jengo la utawala, majengo ya kliniki, warsha, nyumba za watumishi na mengine.

Kwa sasa, majengo mengi ni chakavu na yanahitaji ukarabati mkubwa. Kutokana na upungufu wa kifedha hospitali haijaweza kuweka bajeti ya kutosha ili kufanya shughuli hii kwa muda mrefu, kwa hiyo tunatafuta mfadhili yeyote ambaye yuko tayari kutusaidia katika eneo hili. Miundombinu mingine inajumuisha mifumo ya maji, umeme, na barabara zinazohitaji matengenezo ya mara kwa mara.

Wafanyakazi

Hivi sasa, hospitali ina wafanyakazi 120 wa afya wa kada mbalimbali. Miongoni mwao kuna madaktari 2, madaktari wasaidizi wa afya 4, mtaalamu wa mambo ya ganzi 1 (anesthetist­), madaktari wawili wa muda wa ziada (daktari wa upasuaji na magonjwa ya wanawake).


Huduma zinazotolewa na Hospitali ya Misheni ya Mbozi

 • Huduma ya meno
 • Matibabu / kliniki ya kisukari (Alhamisi): upimaji wa sukari ya damu, uzito wa mwili na shinikizo la damu. Ushauri kuhusu chakula cha kisukari.
 • Kliniki ya afya ya akili (Jumatano): kifafa, Kichaa (schizophrenia), kuchanganyikiwa (acute psychosis).
 • Idara ya Uzazi salama na Magonjwa ya Wanawake (Obstetrics and Gynaecology) ( + upasuaji wa fistula)
 • Chumba cha upasuaji: upasuaji wa uzazi (caesarean section), upasuaji mdogo (Mini Lap), utoaji wa sampuli (Excisional Biopsy), upasuaji wa sehemu iliyokuwa wazi na kuirekebisha (hernia repair), Laparotomy, Utoaji wa kizazi chenye matatizo (Hysterectomy)
 • Huduma ya macho (Ophthalmic)
 • Huduma ya ufanyishwaji mazoezi maalumu (Physiotherapy)
 • Huduma ya mionzi (Radiology)
 • Kifua kikuu na Ukoma
 • Afya ya uzazi kwa vijana: Kuongeza ufahamu juu ya magonjwa ya zinaa na VVU, mimba isiyotarajiwa, utoaji wa mimba salama, huduma baada ya kutoa mimba, uzazi wa mpango, utoaji wa kondomu.
 • Programu ya VVU / UKIMWI 
  • Ushauri nasaha na Upimaji (VCT)
  • Kuwaelimisha watu wanaoishi na VVU baada ya kupimwa (PTC & PLWHA)
  • Uhudhuriaji wa kila mwezi kwa watu wenye VVU + juu ya matumizi ya ARV 
  • Kliniki ya matibabu na uangalizi maalumu (care and treatment unit)
 • Kumfariji mgonjwa bila kupata matibabu yoyote mfano mtu mwenye kansa (Palliative Care (HBC: huduma ya nyumbani): kuwasaidia watu juu ya lishe, dawa, na shughuli zinazozalisha kipato
 • Kuzuia maambukizi kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto (PMTCT): matibabu kabla na baada ya kujifungua, na ufuatiliaji 
 • Huduma ya afya ya mama na mtoto: hutoa huduma ya uzazi na njia za uzazi wa mpango 
 • Kitengo cha upimaji wa magonjwa ya zinaa (STI & RTI): Elimu ya afya, kinga shuleni, usimamizi wa magonjwa, ushauri nasaha 
 • Watoto Yatima na wanaoishi katika mazingira magumu VVU (OVC): Kituo cha yatima kwa watoto 12 tangu kuzaliwa hadi umri wa miaka 
 • Huduma za Maabara (Laboratory services): Idara ya damu (Haematology), uongezaji damu (blood transfusion), Serology, upimaji wa bakteria (Bacteriology), upimaji wa kikemia (Biochemistry), upimaji wa wadudu mbali mbali (Parasitology), Microbiology
 • Kitengo cha dawa (Pharmacy)
 • Huduma za kiroho: ibada kila siku asubuhi na Jumapili. Hospitali ya Chaplain huwatembelea wagonjwa kutoa huduma za kiroho, ushauri nasaha. 

Mtazamo

Jamii yenye afya inayochangia kwa ufanisi maendeleo ya watu na Taifa.

Lengo

Kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kuwezesha utoaji wa huduma za msingi za afya zenye ubora, huduma za kukinga na kutibu.


Mawasiliano

Hospitali ya Misheni ya Mbozi 

S.L.P. 340
Mbozi-Songwe
Tanzania

Simu:   +255 756 269 085
        +255 762 031 143
Barua Pepe:  missionhospital@yahoo.com
Kiswahili