Kituo cha afya cha Nkanga

Kituo cha Afya cha Nkanga kilianzishwa mwezi Oktoba 1998 kwa msaada wa Mission 21 kutoka Uswisi na chini ya usimamizi wa Mch. Presswork na Maria Rhonner. kinaendeshwa chini ya mwavuli wa Hospitali ya Misheni ya Mbozi, kwa lengo la kutoa huduma za afya za msingi katika maeneo ya mbali ya kata ya Itaka, kilomita 30 kutoka Hospitali ya Misheni ya Mbozi. Huduma kuu zinazotolewa ni afya ya uzazi na mtoto, matibabu ya matatizo madogo ya afya pamoja na uboreshaji wa afya. Hivi sasa, wafanyakazi nane wanafanya kazi huko. Kuna afisa tabibu, wauguzi wawili, mtaalamu wa maabara, mhudumu mmoja wa afya na wafanyakazi watatu wasaidizi.


Mawasiliano

Kituo cha afya cha Nkanga

S.L.P. 379
Mbozi-Songwe
Tanzania

Phone:   +255 769 636006
Kiswahili