Zahanati ya Iyendwe

Zahanati ya Iyendwe iko katika kijiji cha Iyendwe, wilayani Momba. Ilijengwa kwa msaada wa mradi wa ‘Family Aid’ uliofadhiliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) mwanzoni mwa miaka ya 1970. Lengo kuu la kuanzisha zahanati lilikuwa kuleta huduma kwa watu wa maeneo ya mbali iil kuwawezesha watu kupata huduma kwa ukaribu Pia ilianzishwa ili kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga katika kijiji. Huduma kuu zinazotolewa ni afya ya uzazi na mtoto, matibabu ya matatizo madogo ya afya pamoja na uboreshaji wa afya. Kituo kimeajiri watu wanne; Tabibu msaidizi mmoja, muuguzi mmoja / mkunga na wahudumu wawili wa afya.


Mawasiliano

Iyendwe Dispensary

Simu:
Kiswahili