Zahanati ya Kapele

Zahanati ya Kapele inapatikana Kapele, katika wilaya ya Momba. Ilijengwa kwa msaada wa mradi wa ‘Family Aid’ uliofadhiliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) mwanzoni mwa miaka ya 1970. Lengo kuu la kuanzisha zahanati lilikuwa kuleta huduma kwa watu waishio maeneo ya mbali na kuwawezesha watu kupata huduma kwa ukaribu. Pia ilianzishwa ili kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga katika kijiji. Huduma kuu zinazotolewa ni afya ya uzazi na mtoto, matibabu ya matatizo madogo ya afya pamoja na uboreshaji wa afya. Kituo kimeajiri watu wanne; msaidizi mmoja wa kliniki, muuguzi mmoja / mkunga na wahudumu wawili wa matibabu.


Mawasiliano

Kapele Dispensary
Simu:

Kiswahili