MVTC – Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi Moravian

Chuo cha Mafunzo ya Ufundi cha Moravian (MVTC) kilianzishwa mwaka 2000 jijini Mbeya, Old Forest, Kadege. Kimesajiliwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA). Lengo la shule ni kuandaa kizazi cha vijana wa Kitanzania, bila kujali jinsia wala dini, kupata elimu zaidi, elimu ya kiufundi kwa kiwango cha kitaifa na ajira endelevu. Ndiyo maana, tunafundisha pia ujuzi wa maisha na ujasiriamali katika kozi zetu zote. Chuo kina uwezo wa wanafunzi 450, kwa sasa wanafunzi 400 wamesajiliwa (2019).

Tunatoa kozi za muda mrefu katika taaluma zifuatazo:

  • Useremala na Uundaji 
  • Ufundi wa magari 
  • Ufundi umeme wa magari 
  • Ufundi umeme wa majumbani (pia nishati ya jua kwa wanafunzi wa ngazi ya juu) (DEI)
  • Kozi ya uhadhiri
  • Upishi 
  • Ushonaji na ubunifu wa mavazi

Kozi hizi zinatolewa kwa kipindi cha miaka miwili. Tunaendesha Mitihani ya Taifa ya Msingi (National Based Exams) na Tathmini ya Msingi ya Uwezo (Competence Based Assessments) katika chuo chetu na tunawaandaa wanafunzi wetu kwa Mitihani ya Taifa. Kila mwanafunzi anapata zana za msingi anapomaliza masomo yake ili aanze biashara yake mwenyewe (kama vile mashine ya kushonea kwa washonaji).


MVTC pia hutoa kozi za muda mfupi katika taaluma zifuatazo:

  • Kozi ya mafunzo ya kompyuta (muda unategemea programu)
  • Kozi ya udereva (wiki 5)
  • Kozi ya kiingereza (miezi 3)
  • Uendeshaji wa hoteli na Utalii (miezi 3 hadi 9)
  • Ushonaji (miezi 6)
  • Ufundi umeme wa majumbani (miezi 6)
  • Ufundi wa magari (miezi 6)
  • Ufundi umeme wa magari (vyombo vya moto) (miezi 6)
  • Useremala na uundaji (miezi 6)

Vifaa

Tunatoa vifaa mbalimbali ili kuboresha uzoefu wa kujifunza katika kituo chetu. Kuna mabweni ya wavulana yenye uwezo wa wanafunzi wapatao 50, kwenye eneo la chuo. Pia kuna mabweni ya wasichana yenye uwezo wa wanafunzi 120.

Chuo kina maabara mbili za kompyuta zenye kompyuta zipatazo 50, mtandao wa intaneti (wireless) na vifaa vingine muhimu vinavyotuwezesha kutoa mafunzo ya kitaaluma katika programu ya kompyuta. Kuna jiko lililokamilika kwa ajili ya kozi ya upishi na gereji kwa mafundi wa magari na kozi za ufundi wa umeme. Zaidi ya hayo, kuna maktaba yenye vitabu na kompyuta inayotumiwa na wanafunzi. Pia kuna mtandao wa intaneti kwenye maktaba.

Pia, Chuo cha Ufundi cha Moravian kina vitengo viwili vya uzalishaji. Kitengo cha useremala hutengeneza samani (kwa ajili ya ofisi, shule, mabweni na kampuni binafsi). Pia, kuna waajiriwa tisa wa vitengo vya utengenezaji wa majeneza, mizinga ya nyuki na fanicha mbalimbali. Kitengo cha ushonaji kimejikita katika ushonaji wa sare ( za wanafunzi, wachungaji na siku za mahafali), pia nguo binafsi

Staff
Mkuu - Gad LwingaMratibu wa Mafunzo - Shadrak GondweMhasibu - Barnabas Mwang'ondaMhasibu Msaidizi - Famuel  Mwandeko

Mtazamo

1. Vijana bila kujali jinsia wanawezeshwa kuja kujiajiri.

2. MVTC kinajiendesha kwa rasilimali zake na msaada kutoka kanisani.

3. Kampuni ndogo ndogo za kibiashara zilizopo zinawezeshwa


Mawasiliano


MVTC - Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi Moravian

S.L.P. 152
Mbeya
Tanzania

Barua Pepe:    mvtcmbeya@gmail.com
Simu:     +255 025 2503272
         +255 755 766 862



Kiswahili