Idara ya Hospitali na Magereza

Idara ya Gereza na Hospitali ilianzishwa kwa mujibu wa dhana ya kibiblia "nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia." (Mathayo 25:36)

Kazi ya mchungaji wazamu ni kuhubiri injili, kuombea wagonjwa na kutoa ushauri nasaha kwa wafungwa. Wajibu mwingine wa mchungaji kuwafundisha wafungwa namna ya kujitegemea. Mara baada ya kuwa huru, waweze kufanya kazi wenyewe. Kazi ya tatu  kuwasaidia wafungwa kwa kuwapa nguo, sabuni, bidhaa za usafi, Biblia na vitabu vya nyimbo.

Huduma hii hutolewa na jimbo ilianza mwaka 1999, na wachungaji wa sasa ni Mch. Stephano Ngondya aliyehudumu miaka 14 na Mch. Ambukege Mwaihoba.

Magereza yanayohudumiwa na wachungaji ni:

  • Songwe (wafungwa 357)
  • Ilembo (wafungwa 270)
  • Mbalali (wafungwa 102)
  • Ngwala (wafungwa 65)
  • Ruanda (wafungwa 1500)
  • Mkwajuni (wafungwa 20)

Mafanikio

Injili ya Yesu imekuwa ikihubiriwa kwa wafungwa, ambapo watu wa dini nyingine wamebadilishwa na kuwa Wakristo.

Changamoto

  • Wafungwa hawana mablanketi ya kutosha, mashuka, sabuni na Biblia.
  • Ukosefu wa usafiri kwa wachungaji walio zamu. Njia nzuri ya usafiri inabidi liwepo gari.
  • Umbali wa kwenda magereza, kwa mfano gereza la Nguala ni kilomita 258 kutoka Mbeya.

Matarajio

Matarajio yetu kuhakikisha kwamba wafungwa wanakuwa raia wema, na kulitumikia Taifa na kanisa pia.

Mapendekezo

Tunapendekeza kwamba Wakristo watoe msaada kwa wafungwa kama vile nguo, viatu, mablanketi, sabuni na bidhaa za usafi



Mkuu ya Idara - Stephano Joseph Ngondya
Mawasiliano

Kanisa la Moravian Tanzania - Jimbo la Kusini Magharibi
Idara ya Gereza na Hospitali

S.L.P. 377
Mbeya
Tanzania

Simu:  +255 752 334625
Kiswahili