Idara ya Umoja wa Wanaume


Idara hii ilianzishwa kutokana na maagizo ya sinodi ya kanisa iliyofanyika mwaka 2016. Sinodi iliagiza kwamba kuwepo na Idara ya Wanaume. Katibu wa Idara hii ni Mchg. Anyandwile Kajange. Wanachama wa idara hii ni wanaume wote katika jimbo wenye ndoa na wasio na ndoa pamoja na wachungaji.

Dira /Mtazamo (Vision)
Kufanya mbingu, kutengeneza mazingira ambayo wanaume wanamotishwa na kutiwa moyo kuendeleza uhusiano wao na Yesu Kristo na wanahimizwa kugundua, kuendeleza na kutumia vipawa vyao vya kiroho na kimwili kutumika katika utume wa Bwana wetu Yesu Kristo - Matt. 28: 19-20


Dhima (Mission)
Kukamata mioyo ya wanaume kwa injili, kuwatia moyo wanaume kushiriki katika shughuli za ushirika ambayo zitawawezesha kuwa viongozi watumishi wa kweli katika familia, kanisa, mahali pa kazi na jamii kwa ujumla.

 Maadili ya Msingi
(Core Values)
  • Uaminifu
  • Kuwa na bidii
  • Kujitolea
 Malengo
  • Kunyenyekea kwa kundi la kichungaji katika kuendeleza maono ya Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi
  • Katika mikutano yetu tunalenga kushirikiana pamoja tunapojifunza Neno la Mungu ili tuwe tumeiva kujilisha wenyewe, familia zetu na wengine kutokana na maandiko matakatifu.
  • Kusaidiana katika maombi na ujirani mwema
  • Kuweka wanaume pamoja katika kujifunza Biblia, huduma, faragha, na uwajibikaji
  • Kuwahimiza na kuwafundisha wanaume kanuni ya  uwajibu wao kibiblia
  • Kuitikia mahitaji ya wanaume ya kiroho kwa kumweka Kristo katikati kwa maendeleo ya kiroho
  • Kuwa watumishi wa kweli kama Mungu alivyotuita kutumikia wengine kama yeye alivyotumika Marko 10:42-45
  • Kufanya mambo yote kwa ubora kwa sababu sisi ni wakilishi wa Mungu
Kitambulisho (Motto)
"Sisi ni Askari wa Kikristo wa Kweli."
Katibu wa Idara ya Umoja wa Wanaume - Anyandwile Kajange

Mawasiliano

Kanisa la Moravian Tanzania - Jimbo la Kusini Magharibi
Idara ya Umoja wa Wanaume

S.L.P. 377
Mbeya
Tanzania

Simu: +255 763 943101


Kiswahili