Moravian SACCOS

Kikundi cha Akiba na Mikopo "Moravian Saccos LTD" ni benki isiyo rasmi inayosaidia mahitaji ya wafanyakazi wa kanisa. Kwa sababu mfumo rasmi wa benki hautoi mikopo midogo, Saccos ni suluhisho kwa kukopesha fedha wafanyakazi wa kanisa. Matumizi ya hii mikopo midogo ni kwa ajili ya mahitaji kama vile ujenzi, ada za shule, kilimo au kuanzisha biashara ndogo, kama ufugaji wa wanyama. Licha ya juhudi zetu nzuri, mahitaji yamekuwa makubwa kuliko fedha zinazokusanywa na Saccos kwa kuwa kuna wafanyakazi 300 wa kanisa. Matokeo yake, mfumo hauwezi kuidhinisha maombi yote. Wadau wanakaribishwa kuunga mkono juhudi za mradi wa SACCOS.


Mawasiliano

Moravian SACCOS LTD.

S.L.P. 3078
Mbeya
Tanzania

Simu: +255 756 855950
Kiswahili