Msaada wa Kisheria

"Everyday Justice for Everyday Problems"

Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini-Magharibi mwa Tanzania limejifunza kupitia shughuli zake katika mikoa mingine ya Tanzania kwamba wanawake, watoto na makundi mengine ya watu waishio katika mazingira magumu mkoani Songwe wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa msaada wa kisheria na kukosa uelewa kuhusu haki zao na wapi wanaweza kuzipata haki zao. Hivyo, tangu mwezi Januari 2017 hadi sasa, Kanisa la Moravian jimbo Kusini-Magharibi mwa Tanzania, kwa kushirikiana na LSF, limekuwa likifanya kazi kubwa ya kuwajengea uwezo watu wa vijijini na mijini. Tunalenga kuhakikisha kwamba elimu ya kisheria na msaada wa kisheria unapatikana na unafikika kwa watu wote, hasa kwa wanawake. Mradi umelenga katika upatikanaji wa haki kwa wote, kuhusiana na matatizo ya ardhi, GBV, VAC, migogoro ya wafanya kazi, urithi, ndoa, kesi za madai na jinai hasa kwa wanawake mkoani Songwe.

Huduma zetu:

  • Utoaji wa huduma halali za kisheria kwa wateja – Wasaidizi wa wanasheria hupokea wateja wenye matatizo ya kisheria, wanawashauri na kutatua migogoro ya kisheria kwa kutumia njia mbadala za usuluhishi wa migogoro. Kesi nyingi hutatuliwa, baadhi zinapelekwa katika mihimili mingine ya haki. Pia, wanasaidia wateja kwa kufuatilia kesi zilizopelekwa katika mahakama za rufaa na kuwashauri  wateja wao ipasavyo.
  • Utoaji wa elimu ya kisheria na uelewa - Elimu ya jumuiya hutolewa kwa njia mbalimbali, kama baraza la migogoro la kata, vilabu vya shule, sherehe za umma, mikutano ya kijiji, VICOBA, mikutano ya kidini, makundi ya kidini (vikundi vya wanawake), vikundi vya vijana, vikundi vya waimbaji , Makundi ya shule za Jumapili, makundi ya kiinjilisti, mikutano ya wakulima na mingine. Mada zinazojadiliwa wakati wa utoaji wa elimu ya kisheria ni pamoja na masuala ya ardhi, ndoa, GBV, matunzo ya watoto, urithi, haki za wanawake, ujasiriamali, haki za kibinadamu na katiba.
  • Mafunzo na ufuatiliaji wa wasaidizi wa wanasheria

Utawala

Mkurugenzi MtendajiMratibuAfisa Ufuatiliaji na TathminiMhasibu
Rev. Willey MwasileNsevilwe MsyalihaIsabella KaongaMwitishilwa Kalengo


Mawasiliano

Legal Service Facility - Kanisa la Moravian Tanzania - Jimbo la Kusini Magharibi

S.L.P. 377
Mbeya
Tanzania

Barua Pepe:    moravainparalegal@gmail.com
Simu:      +255 754 516170
          +255 763 986859
Kiswahili