Ofisi Kuu

Ofisi yetu kuu inapatikana Mbeya barabara ya Jacaranda, katika ploti namba 215, karibu na Shirika la utangazaji Tanzania (TBC).

Kuna kanisa linaitwa usharika wa Jacaranda na nyumba za makazi za kamati tendaji.

Isitoshe, kuna ofisi za idara mbalimbali kama vile Dawati la HIV, idara ya Vijana na nyinginezo. Pia, kuna hosteli ya Vijana ya Moravian na duka.

Muundo wa shirika

Katika ngazi ya jimbo, muundo wa kanisa umegawanyika katika Kamati tendaji (EXCO) yenye Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Askofu na idara kumi na nne (14). Kila moja wapo inaongozwa na karani. Pia, muundo huu upo katika ngazi ya wilaya, mkoa na usharika.


Mawasiliano

Kanisa la Moravian Tanzania - Jimbo la Kusini Magharibi
Head Office

S.L.P. 377
Mbeya
Tanzania

Barua Pepe:    mctswp@yahoo.com
Simu:      +255 025 2502643
Kiswahili