Shirika


Jimbo la Kusini- Magharibi lina ziadi ya shirika 133. Baadhi ya shirika hizo, ni za zamani sana, kama vile usharika wa Utengule, ulianzishwa mwaka 1895 na Wamisionari Wajerumani. Ni usharika wa zamani zaidi katika jimbo la Kusini – Magharibi.

Usharika wa Mbozi ni usharika wa pili wa zamani katika jimbo la Kusini – Magharibi. Ulianzishwa na wamisionari wajerumani, miaka michache baada ya usharika wa Utengule, katika mwaka 1899.

Kuna shirika nyingi za vijijini ili kufikia idadi ya watu katika vijiji, mojawapo ni Gua.

Mwisho, kuna shirika nyingi za mijini, kama ulio  katika Ofisi yetu kuu katika Jacaranda.

Kiswahili