Matukio Yajayo

  • Mbaraka wa Wachungaji katika ushirika wa Mabatini  tarehe  3 Novemba, 2019
  • Sinodi ya Katiba katika ushirika wa Mabatini  kuanzia tarehe 4 Novemba, 2019 hadi 6 Novemba, 2019


Matukio ya hivi karibuni

  • Mbaraka wa Wachungaji katika Ushirika wa Mbatini. wachungaji, wainjilisti na ndugu walianza mfungo wao katika Hostel ya Jimbo kuanzia tarehe 29/10/2019 hadi 02/11/2019.
  • Wanambaraka walifanya mfungo wao katika Hostel ya Moravian - Jacaranda. Hivyo  waliobarikiwa kuwa mashemasi walikuwa watatu (03) akiwemo mwanamke mmoja (01) na waliobarikiwa kuwa makasisi walikuwa wachungaji nane (08).
  • ibada ya Mbaraka wa Wachungaji ilifanyika katika ushirika w mabatini tarehe 03/11/2019 ikiongozwa na Mchg. Zakaria Sichone na Askofu Dkt. Alinikisa F. Cheyo akiwawekea mikono.
Mashemasi wakibarikiwa
    • Mazishi ya Mariam Cheyo, mke wa Askofu wa sasa wa Kanisa la Moravian nchini Tanzania – Jimbo la Kusini-Magharibi, tarehe 13 Juni 2019 katika usharika wa Yerusalemu, Mbeya
Kuagwa kwa Ndugu Etienne Jenni MVTC na Makao Makuu
KMT-JKM iliandaa tafrija fupi kwa ajili ya kumwaga ndugu Etienne Jenni aliyefanya nasi kama mtengenezaji wa tovuti ya kanisa na kompyuta. Alianza kufanya kazi Novemba 3, 2018 hadi Julai 1, 2019. Tafrija zilifanyika Chuo cha Ufundi Moravian tarehe 25.06.2019 na Makao Makuu tarehe 27.06.2019
KMT-JKM inamtakia safari njema kurudi kwao Uswissi.
25.06.2019 katika Chuo cha Ufundi Moravian
27.06.2019 katika Makao Makuu Jacaranda

Kozi ya Ufumaji masweta na Ushonaji

Darasa la awamu ya saba limefanya mahafali yake leo tarehe 29 Juni,2019 hapa Jacaranda. Darasa linaendeshwa na Idara ya Umoja wa Wanawake na Watoto na kufadhiliwa na Mission 21.
Wanafunzi wa darasa hili walianza 24 na mwisho wa mafunzo yao walifanikiwa kumaliza wanafunzi 19.
Hotuba ya wahitimu  29.06.2019wahitimu wa awamu ya sita

TANZIA
Mch. Fedson F. Mwashilindi
Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi limepoteza Mwenyekiti na mchungaji wa Wilaya ya Chunya Mch. Fedson F. Mwashilindi tarehe 24/07/2019. Mchungaji amefia katika Hospitali ya Muhimbili huko Dar es Salaam.
Mazishi yatafanyika tarehe 27/07/2019 katika mji wa Vwawa, Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe.

IBADA YA MAZISHI 
Matukio Katika Picha


MATUKIO YA MBARAKA NA SINODI YA KATIBA
mbaraka wa wachungaji ulifanyika katika Ushirika wa Mabatini tarehe 03/11/2019. kabla ya mbaraka huo wachungaji, ndugu na wainjiisti walikuwa na mfungo wa siku nne (4) kuanzia tarehe 29/10/2019 hadi tarehe 02/11/2019.

Mfungo uliongozwa na Askofu Dkt. Alinikisa Cheyo na viongozi wa Kamati Tendaji. waliopata mbaraka wa Ushemasi walikuwa watatu (03) kati yao akiwepo mwanamke mmoja. waliopata mbaraka wa Ukasisi walikuwa wachungaji wanane (08).

Ibada ya mbaraka wa wachungaji iliongozwa na mwenyekiti wa Jimbo Mchg. Zakaria Sichone na Askofu Dkt. Alinikisa Cheyo aliwawekea mikono waliobarikiwa.
Kiswahili