Chuo cha Ualimu cha Moravian

Baada ya serikali kuzindua kampeni "shule moja kwa kila kijiji" mwaka 2000, shule nyingi zilijengwa. Kwa bahati mbaya, idadi ya walimu haikukidhi mahitaji. Kulikuwa na ongezeko kubwa la mahitaji ya walimu wenye sifa. Kwa kukabiliana na hitaji hilo, Chuo cha Ualimu cha Kanisa la Moravian kilifunguliwa jijini Mbeya mwaka 2009.

Mwezi Januari 2019, wanafunzi wapatao 80 walisajiliwa na zaidi ya wakufunzi 10 walikuwa wakifanya kazi shuleni. Tunatoa Astashahada ngazi ya elimu ya msingi kwa miaka miwili na Shahada ngazi ya elimu ya sekondari kwa miaka miwili.


Utawala

Mkuu Makamu Mkuu

Mtaaluma mkuu

Edina MwakyambikiJulius MwakyusaSalima Amos

Motto wa chuo: Elimu ni maendeleo

Mtazamo: Kuwa na chuo cha kijumuiya chenye uwezo, hali na wajibu wa kushiriki kikamilifu katika nyanja zote kiroho, kijamii, kisiasa na kiuchumi kwa maendeleo ya chuo na Taifa kwa ujumla.

Lengo: kuhakikisha mazingira mazuri ambayo huwawezesha walimu - wanafunzi kuwa walimu wazuri wenye tabia njema na maadili popote wanapohudumia.Mawasiliano

Chuo cha Ualimu cha Moravian

S.L.P. 1454
Mbeya
Tanzania

Simu:     +255 764 838315
      +255 754 574272
Kiswahili